Download Swahili brochure (PDF, 466KB)
Jinsi ya kufanya malalamiko kuhusu huduma yako ya usaidizi wa ulemavu.
Wakati mwingine watu hawana furaha kuhusu huduma yao ya msaada wa ulemavu.
Wewe unaweza kumwambia Kamishna wa Huduma za Ulemavu ikiwa unataka kuzungumza na mtu kuhusu huduma ya msaada wa ulemavu katika eneo la Victoria. Pia wewe unaweza kuuliza familia yako au marafiki wako kukusaidia kuzungumza na sisi.
Sisi tutafanya kazi na wewe pamoja na huduma ya msaada ili kufanya mambo vizuri. Huduma yetu ni bure kabisa na inajitegemea kutoka serikali na huduma zingine.
Watu wengine wanahitaji mkalimani ili waweze kutumia lugha isiyo ya Kiingereza wakati wa kuzungumza na sisi. Sisi tunaweza kukupangia mkalimani wa bure.
Ili kuzungumza na sisi:
-
Tupigie simu kwenye nambari 1800 677 342 au kwa kujaza fomu hapa chini. Tuambie ikiwa unahitaji mkalimani. Sisi tunaweza kukuita tena kwa kutumia mkalimani.
-
Tuambie nini kinachokufanya wewe usiwe na furaha.
-
Tunaweza kuamua pamoja na wewe, nini cha kufanya baadaye.